30 Machi 2017

DC-MJEMA ARUDI KUKAGUA UKARABATI WA SHULE ILIYOHARIBIWA NA UPEPO

Na: Hashim Jumbe
Miongoni mwa athari zilizosababishwa na upepo mkali ulioambatana na mvua zilizonyesha Jumatatu ya tarehe 06 Machi, 2017 kwenye maeneo ya Kata za pembezoni mwa Manispaa ya Ilala ni kuharibika vibaya kwa madarasa matatu, ofisi ya Walimu na miundombinu mingine kwenye shule ya msingi Kigogo Fresh, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe, Sophia Mjema alitembelea shuleni hapo na kujionea athari hizo na kisha kutoa agizo la ukarabati wa haraka kwa jengo hilo.

Tarehe 29 Machi, 2017 Mhe. Mjema ametembelea shuleni hapo na kujionea ukarabati uliofanyika wa jengo hilo uliotumia jumla ya shilingi Milioni 42.

"kutokana na maagizo niliyoyatoa, natumaini hadi kufikia Ijumaa madarasa yatakuwa yamekamilika na siku ya Jumatatu wale Wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili tuliowapumzisha nyumbani kupisha ukarabati huu wataanza kuyatumia madarasa" alisema Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Mjema
Jengo la shule ya msingi Kigogo Fresh lililoathiriwa na upepo mkali na mvua iliyonyesha tarehe 6 Machi,2017 lilivyokuwa linaonekana kabla ya kufanyiwa ukarabati

Muonekano wa sasa wa jengo la madarasa na ofisi iliyoathiriwa na upepo na mvua shuleni Kigogo Fresh baada ya kufanyiwa ukarabati
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema akizungumza na Walimu shuleni hapo mara baada ya kufanya ukaguzi wa jengo la madarasa na ofisi
Wakati huohuo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Mjema aliitembelea familia iliyompoteza Mama yao kufuatia kuangukiwa na mti mkubwa uliosababishwa na mvua na upepo iliyonyesha siku ya Jumatatu maeneo ya Majohe-Bombambili

29 Machi 2017

MKAKATI WA UKUSANYAJI WA MAPATO KWA NJIA YA ELETRONIKI KATIKA KUONGEZA MAPATO YA HALMASHAURI

Na Neema Njau

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala yaendesha mafunzo ya utumiaji wa vifaa vya kieletroniki vya kukusanyia mapato (POS Mashine) kwa watendaji wa Kata pamoja na watumishi walio katika ofisi za Kata.
Akifungua Mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Bibi Tabu F. Shaibu Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala alitoa wito wa Matumizi sahihi ya mashine za POS  ili kuleta  tija na ufanisi katika makusanyo ya mapato ya Halmashauri.
Aliendelea kueleza kuwa mafunzo hayo ni Muhimu na yatatatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zinajitokeza wakati wa utumiaji wa POS Mashine  katika utekelezaji wa majukumu ya kukusanya mapato ya Halmashauri.27 Machi 2017

ENEO LA MIKOKO LA DARAJA LA SALENDER LAFANYIWA USAFI


Na Tabu Shaibu
Katika utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Mghufuli  wa kuliweka Jiji la Dar es salaam katika hali ya usafi, Wanafunzi na Walimu wa Shule ya uuguzi kutoka Hospital ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala walishiriki zoezi la usafi lililofanyika katika eneo la Daraja la Salender. Zoezi hilo lililofanyika Jumamaosi ya tarehe 25/03/2017 lililenga kuondoa taka zilizolundikana kwenye miti ya mikoko  iliyopo eneo hilo. Umuhimu wa usafi huo ni kuhakikisha mazalia ya viumbe hai yanatunzwa.


15 Machi 2017

KAMATI YA FEDHA NA UONGOZI MANISPAA YA TEMEKE WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO MANISPAA YA ILALA

Na: Hashim Jumbe
Kamati ya Fedha na Uongozi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, leo imefanya ziara ya mafunzo kwenye Halmshauri ya Manispaa ya Ilala na kupata elimu namna gani Manispaa ya Ilala inavyokusanya mapato hususani kwenye eneo la masoko, ambapo Manispaa ya Ilala iliwaeleza namna bora ya ukusanyaji mapato kwenye masoko ikiwa ni pamoja na njia ya kutumia wawekezaji wa nje kukusanya ushuru.

Mbali na kuwa na shabaha ya kujifunza namna ya ukusanyaji mapato kwenye masoko, Ziara hiyo pia iliakisi mwanzo mwema wa ushirikiano kati ya Halmashauri hizo mbili.